Reading Time: < 1 minute

Aki mimi sitawahi penda tena
sitamani kuambiwa
Napendwa
Wala kujipa kwa mtu
Asilimia mia moja
Aki ya Mungu
Sitawahi penda tena

Kama binadamu mwenzako
anaeza kukuona kama taka
Akurushe kwenye pipa
Aki mimi sitawahi penda tena
Yaani uliniangalia
Ukaona mimi hafifu sana
Pumbavu wa mapenzi yako
Dharau ukaeka mbele
Mimi ukanisahau nyuma
Aki sitawahi penda tena

Mimi binadamu na hisia
Nyingi kuliko zako
Hekima na busara zangu
Nikazitenga
Ili maskio na fikira
Ziende sambamba na ulivyo
Lakini simba marara ukawa
Ukatupa utu wako
Kwa sekunde mbili za raha
zitakazo tenga na kuharibu
Urafiki na uenzi wetu
Aki ya Mungu
Mimi sitawahi penda tena

Mimi mjinga umenisoma
Ukatupilia wendani wetu
Kwa sekunde mbili za ngono
Nikawa nunge kwako
Ukaniona vile babuyo alimwona nyanyayo
Ukanilindima kwa dhuluma
zilizofata nyanya yangu
ukaona yafaa iwe maisha yangu
Io ya karne zilizopita
Dhuluma za jinsia ya kike
We mwandani wangu
Niliyemweka kwa uti wa mtimangu
ukarusha heshima zako kwangu chooni
Ikawa kinyesi
Aki mimi hutaskia mapenzi
mdomoni ikitoka

Kwanza nataka kuhama Nairobi
Mahaba nitapata Mombasa
Ama Azania
Sitawahi penda tena mimi
Nataka kubadii
Nywele rangi
iwe ya damu
Maana damu yangu yamwagika
Yatiririka
Nataka nibadili jina
Iwe tofauti ya ulivyoniita
Nibadili kila kitu
Ulichoshika mwilini
na maishaini

Aki ya Mungu
Mimi sitawahi penda tena
Sitamani kipendwa!
Aki ya Mungu
Sitawahi penda tena
Mimi ata sitamani kupendwa!

 

Gemini Spice 

By Gemini Spice

Creative And Vivacious Poet

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Social media & sharing icons powered by UltimatelySocial